DONDOO YA LEO : NENO LA MUNGU
Neno la Mungu nisilaha tosha kwa kila mkristo. Dunia iliumbwa kwa Neno, Mungu aliwavuvia manabii waliandike Neno ili kila atakae lisoma, aumbwe upya kiroho na kimwili. Laiti kama wanadamu wangeisoma Biblia na kuifanya kua ndio msingi wa maisha yao, leo watu wasingelipotoshwa na manabii wa uongo na makristo wa uongo tunaowaona kila mahali. Watu wamekataa kulisoma Neno na wameweka imani zao kwenye ishara na miujiza, hivyo shetani kwasababu ni malaika alie anguka na anao uwezo wa kutenda miujiza, ametumia nafasi hiyo kupotosha na kudanganya maelfu ya watu kupitia watumishi wake huku wakijifunika katika kifuniko cha ulokole bandia.
#DondooZaPrinceAmos
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment