UJUMBE WA PRINCE AMOS



Katika siku hizi za mwisho Bwana atafanya kazi kwa namna iliyotofauti sana na vile watu walivyodhani. Itakua ni kinyume kabisa na akili ya mwanadamu na utaratibu wa kibinadamu. Sio kila mtu katika zama za zamani za Biblia aliitwa kufanya kazi na Taasisi (Mfumo) uliokuwepo. Ingawa walikuwepo walioitwa kufanya kazi ndani ya System (Kanisa) lakini kuna wengine walipewa kazi tofauti kabisa na Taasisi zilizokuwepo, na watu hao walipitia wakati mgumu sana, kwani watu waliokua kwenye "Mfumo" waliwapiga vita sana. Kwa mfano Yona alitumwa akahubiri injili Ninawi kitu kilichokua tofauti kabisa na utaratibu wa dini na kanisa Yona alilokua akisali. Kwani watu wa Ninawi walikua wakichukiwa sana na Waizraeli, na Waizraeli waliamini kabisa kwamba     watu wa Ninawi wanastahili hukumu za Mungu, hawastahili kusikia habari za Mungu wa kweli, na kusogeleana nao ni kujitia unajisi. Yohana mbatizaji alipoitwa, alifanya kazi nnje kabisa na Kanisa la kiyahudi lililokuwepo. Na ndio maana wakuu wa dini hawakumwamini na ilifikia hatua wakatuma wapelelezi  kuchunguza alikotoka na amepewa kibali na nani!. Viongozi wa Kanisa la wayahudi walidhani kwamba wao tu ndio waliopaswa kumpa kibali Yohana cha kuhubiri. Na ilipaswa Yohana apitie kwanza kwenye shule zao. Ingawa Kanisa lililokuweko lilimkataa Yohana na utume wake, lakini Yohana kwa imani alitimiza kazi Mungu aliyompa na akalala kwa ushindi mkubwa sana. Sio rahisi hata kidogo kazi Bwana aliyonipa kueleweka kwa ndugu zangu wa Yerusalemu, Yesu aliponitokea "aliniambia wazi kwamba nitakutana na upinzani mkubwa sana, watu haswa walio kwenye mifumo ya kidini hawatanielewa, watanipiga vita sana, lakini nikivumilia hata mwisho nitakula matunda ya mti wa uzima na kuyanywa maji ya mto wa uzima". Tayari nimeshalionja joto la jiwe, nimekutana na upinzani mkubwa sana, nimeitwa muasi, niliepotea, nimerushiwa kila maneno ya laana. Lakini Mungu ajuae siri ya roho yangu amekua akinitia nguvu. Kuna wakati nilikata tamaa na kurudi nyuma na nilimwambia Yesu kwamba sitaweza kufanya utume alionipa kutokana na upinzani ninao upata, niliamua kurudi kwenye System (Taasisi) nilikokua natumika mwanzo. Nilimlilia sana Yesu nakumsii sana ampe mtu mwingine maono hayo, lakini Yesu akaniambia maneno haya "Ni wewe tu Amos ndie nimekuchagua ufanye kazi hii, nimekuandaa tangu ulipozaliwa, nimekutengeneza kwa kazi hii, nimekua pamoja nawe kila ulikokwenda, usiogope nitazame mimi utashinda. Peleka ujumbe kwa ndugu zako Rastafarian's (Marasta) na kwa Watoto wanaoishi mitaani, nitakupigania". Kwa machozi mengi niliamua  kuyabeba tena maono Yesu aliyonipa. Na tangu nilipoamua kufanya hivyo moyo wangu umekua na Amani. Nilienda tena mlimani kwenye msitu kufanya maombi, nikakaa siku 90 nikilala porini na kufanya maombi ya usiku na mchana. Malaika wa Mungu walinitokea marakadhaa na nimepata uthibitisho mkubwa kwamba mbingu yote iko pamoja nami. Ingawa mwili wangu umepungua sana kutokana na maombi ya kufunga kwa muda mrefu sana, lakini roho yangu imejaa moto mkali wenye uwezo wa kuchoma Dunia yote Amen!!!!!

PHOTOS: PERFORMING "KISHA NIKAONA" IN MOROGORO TANZANIA TODAY





Photos when I was ministering through music at central church Morogoro Tanzania, Today

WATCH WAY?.

Enter ye in at the strait gate: for wide is the gate, and broad is the way, that leadeth to destruction, and many there be which go in thereat: because strait is the gate, and narrow is the way, which leadeth unto life, and few there be that find it. Matthew 7:13, 14.OHC 8.1
Before you are two ways—the broad road of self-indulgence and the narrow path of self-sacrifice. Into the broad road you can take selfishness, pride, love of the world; but those who walk in the narrow way must lay aside every weight, and the sin which doth so easily beset. Which road have you chosen—the road which leads to everlasting death, or the road which leads to glory and immortality? OHC 8.2
There never was a more solemn time in the history of the world than the time in which we are now living. Our eternal interests are at stake, and we should arouse to the importance of making our calling and election sure. We dare not risk our eternal interests on mere probabilities. We must be in earnest. What we are, what we are doing, what is to be our course of action in the future, are all questions of untold moment, and we cannot afford to be listless, indifferent, unconcerned.It becomes each one of us to inquire, “What is eternity to me?” Are our feet in the path that leads to heaven, or in the broad road that leads to perdition? ...OHC 8.3
Those who make a success of the Christian life will count all things as loss for the excellency of the knowledge of Christ. Only those who are abiding in Christ can know what true life is. They realize the value of true religion.They have brought their talents of influence and means and ability to the altar of consecration, seeking only to know and do the will of Him who has died to redeem them. They know that the path they must travel is strait and narrow, and that they will have to meet many obstacles and temptations, as they resist the enticements of the broader road that leads to ruin; but they will discern the footsteps of Jesus, and press onward toward the mark for the prize of the high calling in their Lord and Saviour. They will choose the royal way that leads to heaven. OHC 8.4

DEVOTIONAL : Singleness Of Purpose

The light of the body is the eye: if therefore thine eye be single, thy whole body shall be full of light. Matthew 6:22.

This says, “thine eye,” not some other person’s eye. The rich experience that it is our privilege to have, we lose when we expect someone else to do our seeing for us, and guide us in our spiritual experience as if we were blind. We must have a single eye to God’s glory, a single and persistent purpose to leave self and the preferences of others out of the question, not asking, “If I take this course, shall I increase my personal possessions, or shall I decrease them?”
Great simplicity must be cherished by those who seek wisdom of God. Then their feet will not slide. “The path of the just is as the shining light, that shineth more and more unto the perfect day. The way of the wicked is as darkness: they know not at what they stumble.” ...
A person who truly loves and fears God, striving with singleness of purpose to do His will, will place body, mind, heart, soul, and strength under service to God. Thus it was with Enoch. He walked with God. His mind was not defiled by an impure, defective eyesight. Those who are determined to make the will of God their own must serve and please God in everything. Then the character will be harmonious and well-balanced, consistent, cheerful, and true.
“But if thine eye be evil,” if you study selfish purposes, and work only to that end, the whole character is defective, the whole body is full of darkness. Such do not look to Jesus. They do not behold His character, and they are not changed into His image. The spiritual vision is defective, and the way from earth to heaven is darkened by the hellish shadow of Satan. So Satan is pleased to have it, for he can lead that person blindfolded to ruin.
“If therefore the light that is in thee be darkness, how great is that darkness!” The conscience is the regulative faculty, and if people allow their conscience to become perverted, they cannot serve God aright. Their object in life shows to the world whether they are Christians or in rebellion against God. Their whole life is a failure. It is distorted and double, and all the faculties are misdirected. The profession may be all right, but the faith is perverted, and this is revealed by the practice, which misleads others. “No man can serve two masters: for either he will hate the one, and love the other; or else he will hold to the one, and despise the other. Ye cannot serve God and mammon.

DONDOO YA LEO : NENO LA MUNGU

Neno la Mungu nisilaha tosha kwa kila mkristo. Dunia iliumbwa kwa Neno, Mungu aliwavuvia manabii waliandike Neno ili kila atakae lisoma, aumbwe upya kiroho na kimwili. Laiti kama wanadamu wangeisoma Biblia na kuifanya kua ndio msingi wa maisha yao, leo watu wasingelipotoshwa na manabii wa uongo na makristo wa uongo tunaowaona kila mahali. Watu wamekataa kulisoma Neno na wameweka imani zao kwenye ishara na miujiza, hivyo shetani kwasababu ni malaika alie anguka na anao uwezo wa kutenda miujiza, ametumia nafasi hiyo kupotosha na kudanganya maelfu ya watu kupitia watumishi wake huku wakijifunika katika kifuniko cha ulokole bandia. #DondooZaPrinceAmos

DONDOO YA LEO : MUNGU ANAPOKUPA KAZI

Mungu anapokupa kazi ifanye kwa moyo wako wote bila kuangalia watu wanazungumza nini juu ya utume wako.  Sio kila mtu atakuelewa. Wengine watakupinga na kukuona umepotea lakini kamwe usisikilize maneno yao,  wewe badala ya kusikiliza watu wanaopatwa na mauti na kutoweka, msikilize Mungu anaeishi milele kwenye nuru usiyokaribiwa na giza
#DondooZaPrinceAmos

DONDOO YA LEO : JINA LA YESU

Jina la Yesu lina nguvu kubwa kuliko akili za mwanadamu zinavyoweza kuelewa. Lina mamlaka kamili ya Mungu. Linauwezo wa kuchoma magonjwa, mapepo, hata shetani mwenyewe hawezi kusimama wakati jina la Yesu linapotajwa kwa imani na katika roho.  Jina la Yesu ningao salama wenye haki hukimbilia wakawa salama
#DondooZaPrinceAmos

DONDOO YA LEO: MAOMBI NA KUIMBA NYIMBO ZA SIFA

Kadiri unavyozidi kumkaribia Yesu kwa njia ya maombi na kufunga ndivyo magonjwa yako yatakavyozidi kukimbia. Kadiri unavyomsifu Yesu kwa njia ya Nyimbo, ndivyo unavyo watia nguvu Malaika wa Mungu wazidi kukupigania. Kuna Nguvu ya ajabu katika maombi, kufunga, na kuimba nyimbo za sifa na za ushindi
#DondooZaPrinceAmos