UJUMBE WANGU
Niwakati sasa umefika kwa Injili ya Yesu Kristo ihubiriwe kwa Ndugu zetu Rastafarians. Yesu amenipatia Utume huo mkuu nami kwafuraha nimeitikia wito nakusema "Mimi hapa nitume Bwana". Nimekubali wito wa Yesu Kristo wa kutumika katika kazi ya Injili, huduma za maombezi, kama Nabii wa Mungu na Mnadhiri wa Mungu. Najua wengi hamtanielewa lakini alie katika roho atanielewa. Ziko roho nyingi zinazoangamia gizani kwa sababu watu wanaoujua ukweli wamekataa kuwapelekea nuru badala yake wamebaki kuhukumu na kutafuta makosa ya watu wengine. Kazi yao nikubebea watu dhambi hatakama ulishatubu na kusamehewa lakini wao hawajui kusamehe. Uzinzi nilioufanya myaka saba iliyopita, waompaka leo hii wananihukumu tu tena na kunisengenya kwa kila mtu na ilhali nilishatubu na Yesu alishanisamehe na kunihesabia haki. Mimi Nasimama na Yesu tu Bila kuogopa chochote. Wito wakua hivi nilivyo sasa (Kuweka Dreadlocks Nadhiri) Kwaajili ya Injili nimeupokea kutoka kwa YESU mwenyewe, nami nasonga mbele nyuma sirudi tena. INJILI IENDE MBELE YESU ANAKUJA TENA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment