NAKULETEA ALBUMS MBILI MPYA


Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu Muumba wa mbingu na nchi  kwa kunipa Uhai, Nguvu, na Afya njema.  Mwaka huu Bwana amenipa kibali cha kutoa Albums mbili pamoja na Video Collection Nyimbo kutoka katika Albums zangu mbali, "DUNIA IMEKWISHA" , "AMENISAMEHE", na "DVD COLLECTION 2" kazi hii ambayo nilianza kuifanya kutoka mwaka 2012 sasa imekamilika na nimatumaini yangu kwamba itabariki maelfu ya watu. Nyimbo hizi Mungu alinipa katika nyakati tofauti tofauti wakati mwingine nikiwa nimelala usiku, wakati mwingine nikiwa napiga guitar, wakati mwingine nikiwa kwenye ibada. Kabla ya kuzitoa nyimbo hizi, nilizisikiliza kwanza kwa muda mrefu na nilipoona zina nibariki na zimejaa nguvu ya Mungu, ndipo nimeona vyema niziweke hadharani. Album hizi kwasasa zinapatikana kwenye mtandao na baadae zitapatikana katika CD. Barikiwa unaposikiliza nyimbo zangu mpya
                               BOFYA HAPA USIKILIZE "DUNIA IMEKWISHA"
                             
                                  BOFYA HAPA USIKILIZE "AMENISAMEHE"

Listen to Bwana Ni Nuru Yngu

EE BABA POKEA SIFA


 Sms AM04 Send it to 22454 to get this song on your phone. This service is for Kenya only